Type to search

‘APP’ Ya Tiktok Yaongoza Kwa Idadi Ya ‘Downloads’ Duniani.

Entertainment Swahili News trending News

‘APP’ Ya Tiktok Yaongoza Kwa Idadi Ya ‘Downloads’ Duniani.

Share

App ya TikTok imeipita App ya Facebook kwa kuwa App iliyopakuliwa na watu wengi zaidi duniani. Awali Facebook ndiyo iliyokuwa ya kwanza kwenye orodha ya upakuzi ikifuatwa na TikTok huku Instagram ikishika nafasi ya tatu.

TikTok ambayo ni app ya China ilipata umaarufu mkubwa mwaka 2020 wakati dunia ilikumbwa pakubwa na janga la virusi vya Covid-19 na kulazimu mataifa mengi ya bara la Ulaya, Asia na Marekani kutangaza marufuku ya
‘Lockdown’ ya kutotoka nje.

Tangu kipindi hicho Tiktok imekuwa ikipata wafuasi kwa wingi siku baada ya nyingine. Nchi ambazo zinaongoza kwa upakuzi wa App ya TikTok ni pamoja na China na Marekani kwa asilimia 15% na 9% mtawalia.

Aidha Facebook, Instagram, Messenger na WhatsApp zipo katika orodha ya App tano bora zinazopakuliwa na watu wengi zaidi duniani. Zingine zilizopakuliwa kwa wingi kufikia Julai 2021 ni pamoja na Snapchat ikishika nafasi ya
sita, huku Zoom na Telegram zikishika nafasi ya Saba na nane mtawalia.

Leave a Comment