Type to search

Brown Mauzo Achora Tattoo ya Vera Sidika

Entertainment Swahili News trending News

Brown Mauzo Achora Tattoo ya Vera Sidika

Share

Msanii Fredrick Mtinda maarufu Brown Mauzo amewasisimua mashabiki zake baada ya kuchora tatu mpya ya jina la mpenzi wake Vera Sidika kwenye mkono wake.

Jina Vera amelichora kwenye mkono wake wa kulia huku Sidika likichorwa kushoto. “Mapenzi yangu kwako yamenifanya nichore tattoo mkononi. Nakupenda Sana baby.” ameandika Mauzo katika ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki walionekana kutofagilia wazo la kuchora tattoo hiyo wakisema uwezekano wa watu wawili wanaopendana kutengana sio wa kupuuza. “sisi kama mafans we can’t wait for jina Sidika kubadilika na
kuwa sadaka ” Aliandika shabiki mmoja kwenye kitengo cha komenti.

Brown Mauzo sio msanii wa kwanza hapa Afrika Mashariki kuchora tattoo ya mpenziye. Nyota wa Bongo flavor Harmonize AKA Konde Boy pia aliwahi kuchora tattoo ya mpenziye wa zamani Kajala ila baadae walitengana.

Hata hivyo kuna baadhi ya wasanii wasiofagilia wazo la kuchora tattoo. Kwa mfano Diamond Platnumz wakati mmoja aliwahi kusema tabia ya kuchora tattoo ni ushamba tu.

Leave a Comment