Type to search

Earthquake Kills 304 in Haiti

Swahili News trending News

Earthquake Kills 304 in Haiti

Share

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry ametangaza hali ya dharura baada ya watu wapatao 304 kuangamia kufuatia tetemeko la ardhi na kujeruhi wengine zaidi ya 1900.

Mamlaka husika nchini humo zimesema tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 7.2M,L  na lilitetemesha kaskazini ya Jamaica na baadhi ya maeneo ya Cuba. Hata hivyo Haiti ndiyo iliyotetemeshwa pakubwa.

Tetemeko hilo limeharibu takriban nyumba 949, makanisa 7, mikahawa 2 ya kifahari na shule tatu. Waziri Mkuu Ariel Henry alitangaza hali ya dharura ya mwezi mmoja mara tu baada ya kuzuru eneo la tukio lililoathirika zaidi.

Jiji la Les Cayes ndilo linakadiriwa kuathirika zaidi kwa idadi ya vifo na makazi ya watu kuharibiwa.

Serikali itagharamia mazishi ya wote waliopoteza maisha.

“Nimeona miili ya watu ikibebwa na maafisa wa polisi huku wengine wakijaribu kuondoa mawe kwa kusadiki kwamba bado kuna wengine walioko chini.” Alisema Jean Marie Simon, mkazi wa Les Cayes ambaye alikuwa sokoni tetemeko lilipotokea.

“Nilikuwa nasikia tu sauti za vilio kila mahali.” Alieleza zaidi Jean Marie ambaye familia yake, mke na mtoto walinusurika kifo.

Aidha serikali ya Haiti imefunga barabara nyingi zinazoelekea Kusini mwa taifa hilo mpaka pale shughuli ya utafutaji wa miili itamalizika.

Kevin Ikaira

Leave a Comment