Type to search

Haiti: Idadi Ya Waliofariki Yafikia 1941.

None

Haiti: Idadi Ya Waliofariki Yafikia 1941.

Share

Idadi ya watu walioaga dunia kwenye tetemeko la ardhi Haiti imefikia watu 1941 huku zaidi ya 10,000 wakijeruhiwa. Aidha,wapo watu wengi wasiojulikana waliko.

Mamlaka zinazosimamia shughuli ya uokoaji zimeeleza miili ya watu inaendelea kupatikana kadri wanavyozidi kufikua vifusi vya nyumba zilizoanguka kufuatia tetemeko hilo. Aidha ufukuaji wa vifusi umekumbwa na changamoto ya Kimbunga ‘Grace’ ambacho wataalam’ wa hali ya hewa wanasema huenda kikavuruga hali hata zaidi.

Umoja wa mataifa UN umesema hospitali karibia zote zimezidiwa na idadi kubwa ya majeruhi wanaohitaji matibabu
ya kina na wengi wanalazimika kulala sakafuni.

Aidha watoto wapatao 500,000 wamepoteza makazi na hawana maji safi ya kunywa. UN kwa ushirikiano mkubwa na serikali ya Marekani wanajitahidi kutoa msaada wa chakula na maji hususan katika mji wa Les Cayes, ambao ni moja kati ya miji iliyoathirika pakubwa na tetemeko hilo.

Ikumbukwe taifa hilo limetoka tu kwenye kipindi cha maombolezo baada ya kuuliwa kwa Rais wao Jovenel Moise.

Leave a Comment