Type to search

Haituhusu! Kenya Yawajibu Raia Wake Waliokwama Afghanistan.

Swahili News trending News

Haituhusu! Kenya Yawajibu Raia Wake Waliokwama Afghanistan.

Share

Wizara ya mambo ya nje kupitia Katibu Mkuu Macharia Kamau imeshauri Wakenya waishio nchini Afghanistan
kufanya mipango yao wenyewe na waajiri wao iwapo wanataka kurejea nyumbani.

Macharia amesisitiza kuwa Serikali ya Kenya Haina mpango wowote wa kuwarudisha nyumbani kwa sababu
Afghanistan na Kenya hazijakuwa na uhusiano wa kidiplomasia kwa muda mrefu.

Aidha Macharia pia amewashangaza Wakenya waliosafiri kwenda Afghanistan ikizingatiwa ni taifa ambalo limekuwa na historia ya vita na ghasia kwa muda mrefu. “Kenya haina uhusiano wa kidiplomasia na Afghanistan. Pili hilo ni taifa ambalo halijakuwa na amani kwa muda mrefu sasa na kwa hivyo hatutarajii Wakenya kusafiri kwenda huko,” Amesema Katibu Mkuu katika Wizara ya mambo ya nje Macharia Kamau.

Pamekuwepo na shinikizo miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii wakiitaka Serikali kuwasaidia Wakenya waishio Afghanistan kwa namna, hali ni tete nchini humo sasa hivi, kufuatia kutwaliwa kwa miji mikuu
na Wapiganaji wa Taliban.

Ikumbukwe nchi jirani ya Uganda tayari imejitolea kuwapa hifadhi wakimbizi wapatao 2000 kutoka nchini Afghanistan. Serikali ya Marekani itakuwa ni mhusika mkubwa katika kuwasafirisha watu hao kutoka Kabul Afghanistan mpaka Uganda.

Kwa sasa taifa la Afghanistan Lipo chini ya utawala wa Taliban baada ya Rais wa Afghan Ashraf Ghani kuikimbia
nchi yake akihofia usalama wake. Inasadikiwa alikimbilia taifa la Kazakhstan.

Leave a Comment