Type to search

Hakainde Hichilema Ndiye Raisi Mpya wa Zambia

None trending News

Hakainde Hichilema Ndiye Raisi Mpya wa Zambia

Share

Tume ya uchaguzi nchini Zambia imemtangaza rasmi Hakainde Hichilema kuwa Rais mteule wa nchi hiyo baada ya kujizolea kura 2,810,777 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Rais Edgar Lungu aliyepata kura 1,814,201.

Hii ni mara ya tano kwa Hakainde Hichilema, maarufu kama HH kuwania nafasi ya kiti cha urais wa taifa hilo. Aidha jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na umoja wa Ulaya EU umesihi Rais aliyeko madarakani Edgar Lungu kukubali matokeo ya uchaguzi Ili kuepuka ghasia.

Awali ofisi ya Rais ilituma taarifa kwa vyombo vya habari ikipinga matokeo walipogundua Hakainde anaongoza kwa kura nyingi. Katika taarifa hiyo ya ikulu ya Rais, Rais Lungu alidai kuwa uchaguzi haukuwa wa huru na haki na
kwamba mawakala wa chama chake cha Patriotic Front walifurushwa nje ya vituo vya kuhesabia kura.

Aidha viongozi wa upinzani wamekanusha madai hayo,“Haiwezekani Rais aliyeko madarakani akashindwa kulinda kura zake mwenyewe wakati yeye ndiye amiri Jeshi Mkuu. Hakuna wizi hapa. Wananchi wanataka Uongozi
mpya.” Amesema katibu Mkuu wa UPND, chama cha HH.

Lungu aliingia madarakani mwaka 2015 na moja ya kero lililozungumziwa zaidi katika kipindi cha kampeni ni deni la taifa huku Upinzani wakisema serikali ya Rais Lungu imeomba mikopo zaidi ya haja.

Haijabainika ni hatua gani serikali ya Edgar Lungu inakwenda kuchukua sasa baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza HH kama Rais mteule.

Leave a Comment