Type to search

Kenya Yapokea Shehena Nyingine ya Chanjo Kutoka Uingereza.

Health & Fitness Swahili News trending News

Kenya Yapokea Shehena Nyingine ya Chanjo Kutoka Uingereza.

Share
Picha kwa Hiisani: MOH

Serikali ya Kenya imepokea shehena nyingine ya dozi 406,000 za chanjo ya Astra Zeneca kutoka kwa Serikali ya Uingereza. Shehena hiyo iliwasili Nairobi Jumanne Agosti 17, 2021 usiku, na kupokelewa na kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Afya Patrick Amoth.

Serikali ya Uingereza mpaka kufikia sasa imetoa mchango wa jumla ya dozi 817,000 kuja Kenya. Shehena hiyo ilisafirishwa kuja Nairobi na UNICEF chini ya mpango mzima wa COVAX.

“Hii sasa ni shehena ya pili kutoka kwa Serikali ya Uingereza na itatusaidia pakubwa katika kufikia azimio letu la kuchanja watu wapatao milioni 10 ifikapo Disemba 2021.” Alisema Daktari Patrick Amoth.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa Uingereza nchini Kenya Julius Court amesema Uingereza inapania kutoa mchango wa dozi milioni 100 kwa mataifa rafiki kabla Juni 2022,“Mchango huu ulifanikishwa pakubwa na ziara ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Uingereza na moja kati ya mambo muhimu aliyojadili na Waziri Boris Johnson ni kuhusu upatikanaji wa chanjo kwa ajili ya watu wa Kenya.” Alieleza Bw. Julius Court.

Serikali ya Kenya mpaka kufikia sasa imetoa chanjo kwa watu wapatao milioni 2.1 na lengo ni kuchanja Wakenya milioni 10 ifikapo Disemba mwaka huu.

Leave a Comment

Next Up