Type to search

Kula Hivi Vyakula Ukiwa na Mimba

Food & Nutrition Swahili News

Kula Hivi Vyakula Ukiwa na Mimba

Share

Kipindi cha ujauzito ni moja kati ya nyakati muhimu zaidi katika maisha ya mwanamke yeyote yule. Ni muda muhimu, sio tu kwa mama lakini zaidi kwa mtoto aliyeko tumboni.

Kwa hivyo basi, lishe bora inakuwa ni suala linalostahiki kupewa uzito mkubwa kwa ajili ya kunawiri kwa mama na kitoto chake mpaka pale muda wa kujifungua utakapowadia.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula muhimu zaidi anavyostahili kula/kunywa mama mjamzito;

  • Maziwa na bidhaa zake kama mtindi(maziwa lala) au ‘yoghurt’ kwa kimombo.
  • Mayai.
  • Jamii ya kunde – yaani bidhaa kama maharagwe, mbaazi, dengu na njugu karanga mara kwa mara.
  • Samaki au dagaa(omena).

Iwapo mama atakuwa na urafiki na vyakula hivi katika kipindi chake cha uja uzito basi inasadikiwa kuwa hata mtoto ataimarika kiafya hata atakapofikia kuzaliwa na mamake.

Kumbuka ni muhimu kwa chakula kuiva vizuri ili kuzuia vimelea vya wadudu. Aidha pia samaki wenye zebaki nyingi ni vizuri waepukwe na mama mjamzito.

Leave a Comment