Type to search

Majina ya Maafisa 6 wa Polisi Wanaohusishwa na Mauaji ya Kaka Wawili Kutokea Embu

Swahili News trending News

Majina ya Maafisa 6 wa Polisi Wanaohusishwa na Mauaji ya Kaka Wawili Kutokea Embu

Share

Maafisa 6 wa Polisi wanaohusishwa na mauaji ya kaka wawili kutoka Embu nchini Kenya leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi mbele ya Hakimu Daniel Ngugi.

Sita hao ni kama ifuatavyo:

  • Benson Mbuthia.
  • Consolata Kariuki.
  • Martin Wanyama.
  •  Lilian Cherono.
  •  Nicholas Sang.
  •  James Mwaniki.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Lydiah Nyamosi umeiomba Mahakama kuwashikilia maafisa hao 6 kwa siku 14 ili kufanya uchunguzi zaidi, “Kuna haja ya kuwasitiri mashahidi kwenye kesi hii ili kusudi waweze kutoa ushahidi zaidi kwa majasusi na upande wa mashtaka,” Amesema Lydiah Nyamosi.

“Tunaiomba mahakama kuagiza kuzuiliwa kwa katika kituo cha polisi cha Capitol Hill huku uchunguzi zaidi ukiendelea.” Alisema kiongozi wa upande wa mashtaka Lydiah Nyamosi.

Leave a Comment