Type to search

Manchester United Yaichachafya Leeds Utd.

Sports Swahili News trending News

Manchester United Yaichachafya Leeds Utd.

Share

Klabu ya Manchester United imeandikisha ushindi mkubwa wa magoli (5 – 1) dhidi ya klabu ya Leeds katika mechi yao ya kwanza msimu huu Uwanjani Old Trafford.

Kiungo wa kati Bruno Fernandes amefunga magoli 3 huku Mason Greenwood na Fred wakicheka na wavu kila mmoja na kukamilisha hesabu ya magoli 5 ya Manchester United. Aidha Leeds wamefungiwa goli lao la pekee kupitia beki Luke Ayling.

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba ameonyesha ubora wake baada ya kutoa ‘assists’ nne katika mechi hiyo. Ikumbukwe hatima ya Pogba iwapo ataondoka Man- utd bado haijabainika japokuwa Uongozi wa Man-utd unatamani asiondoke.

Ligi kuu ya Uingereza EPL msimu 2021/2022 iling’oa nanga jana tarehe 14 Agosti 2021.

Leave a Comment