Type to search

NI KWA NINI MSANII JULIANI ANAHUSISHWA NA KUVUNJIKA KWA NDOA YA GAVANA MUTUA ?

Entertainment Swahili News Trend Explained trending News

NI KWA NINI MSANII JULIANI ANAHUSISHWA NA KUVUNJIKA KWA NDOA YA GAVANA MUTUA ?

Share

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii hususan twitter wameonekana kushiriki pakubwa kwenye tetesi za ni kitu gani hasa kimechochea kutengana kwa Gavana wa Machakos Alfred Mutua na Lilian Ng’ang’a.

Ikumbukwe kwa muda sasa pamekuwepo na tetesi kwamba uhusiano wa Lilian na Msanii wa midundo ya HipHop Juliani haukuwa tu wa kawaida kwani wawili hao walionekana kushiriki kwa kina katika maisha ya kila mmoja.

Hata hivyo hakuna aliyewahi kujibu tetesi hizi ila wameendelea kuonekana wakienda matanuzi (hanging out) pamoja; hivi karibuni wakipokea hata mwaliko kwenda kwenye sherehe kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa  aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga.

Tetesi za uswahiba usio wa kawaida kati ya Juliani na Lilian zimeonekana kuzungumziwa zaidi leo baada ya Gavana Alfred Mutua kuthibitisha kuwa wamefikia wamuzi wa kuvunja ndoa yao kwa maelewano.

Tags:

Leave a Comment