Type to search

ODM Yamtaka Chebukati Ajiuzulu

Politics trending News

ODM Yamtaka Chebukati Ajiuzulu

Share

Chama cha ODM kinachoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Raila Odinga kinamtaka Mwenyekiti wa Tume ya
uchaguzi na mipaka IEBC Wafula Chebukati ajiuzulu. Kwa mujibu wa semi zilizotolewa na Wabunge wa ODM
kwenye ibada ya mazishi ya baba mzazi wa Seneta TJ Kajwang; Mhe. Gladys Wanga na Opiyo Wandayi wamesema Chebukati hana sifa nzuri ya kusimamia uchaguzi mkuu ujao 2022.

“Kwa namna Chebukati aliendesha uchaguzi mkuu wa 2017 mpaka tukafikia hatua ya kuurudia baada ya Mahakama kuubatilisha basi hafai” alisema Mbunge Gladys Wanga. Kenya iliweka historia ya kuwa taifa la kwanza katika
ukanda wa Afrika Mashariki na kati kubatilisha matokeo ya uchaguzi.

Inasadikiwa kwamba semi za Wanga na Opiyo ni semi fiche za chama cha ODM kwamba IEBC wanahitaji Mwenyekiti mpya. Ikumbukwe Rais Kenyatta tayari aliwateua makamishna 4 wapya wa IEBC na wanatarajiwa kuapishwa rasmi hivi karibuni baada ya kumalizika kwa msasa na Bunge la kitaifa.

Kenya itakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu Agosti 2022 huku ikitarajiwa kuwa kinara wa ODM Raila Odinga
atakuwa kwenye mstari wa mbele kuwania nafasi ya urais. Hata hivyo, Raila mwenyewe hajatoa semi za kutia dosari Uenyekiti wa Chebukati japokuwa inasadikiwa ni wazo kubwa katika chama cha ODM kwamba Chebukati
hafai.

Leave a Comment