Type to search

Rais wa Rwanda Paul Kagame Aonyesha Kukerwa Kwake Baada ya Arsenal Kushindwa

Sports trending News

Rais wa Rwanda Paul Kagame Aonyesha Kukerwa Kwake Baada ya Arsenal Kushindwa

Share

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameonyesha kukerwa kwake baada ya ‘washika bunduki wa London’ Arsenal kushindwa na klabu ya Brentford katika mechi ya kwanza kabisa ya ufunguzi wa Ligi ya Uingereza EPL msimu 2021/2022. Brentford iliichachafya Arsenal magoli 2 kwa nunge. Rais Kagame, ambaye serikali yake ni mshirika Mkuu na klabu ya Arsenal, amesema ni wakati mwafaka klabu hiyo sasa itangulize akili ya ushindi zaidi ya biashara.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Kagame amesema Arsenal ni klabu isiyostahiki sifa ya udhaifu na tabia ya kupoteza mechi za kawaida Sana.“Timu inastahili kujengwa kwa maono. Hatufai kukubali udhaifu.HAPANA! Na ndiyo najua hata klabu yenyewe inafahamu ni kina nani wanaobeba aibu ya kushindwa.” Ameandika Rais Kagame kwenye
ukurasa wake wa twitter.

Aidha pia Rais Paul Kagame amedokeza kwamba huenda klabu ya Arsenal inanunua wachezaji wazuri kwa bei ghali lakini hawatekelezi wajibu wao inavyostahili – kuiletea klabu sifa ya ushindi. “Namna moja ya kulishughulikia suala hili ni kuangalia iwapo wachezaji tunaowanunua wanatekeleza wajibu wao ipasavyo.” Ameongeza Rais Kagame.

Ikumbukwe kwamba klabu ya Arsenal imekuwa na sifa ya kutanguliza biashara zaidi ya mafanikio Uwanjani, suala ambalo lilichochea sana kuacha kazi kwa aliyekuwa Kocha Mkuu Arsene Wenger msimu wa 2018/2019.

Leave a Comment