Type to search

Raisi Edgar Lungu wa Zambia Ayakataa Matokeo ya Uchaguzi

Breaking News Politics Swahili News

Raisi Edgar Lungu wa Zambia Ayakataa Matokeo ya Uchaguzi

Share

Rais wa Zambia Edgar Lungu ametuma taarifa kwa vyombo vya habari akisema uchaguzi haukuandaliwa kwa huru na haki.

Moja ya sababu alizotoa ni eti mawakala wa chama chake cha Patriotic Front walifurushwa nje ya vituo vya kuhesabia, na hivyo basi ikawa ni vigumu kwao kushuhudia shughuli ya uhesabu kura.

Matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya uchaguzi yanaonesha kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema wa Chama cha National Development ndiye anayeongoza huku akifuatwa na Rais Lungu.

Shughuli ya uhesabu kura itahusisha hesabu za jumla ya majimbo au maeneo-bunge 150 nchini humo.

Aidha tayari wapo wagombea wa kiti cha urais ambao tayari wameshampongeza Hakainde Hichilema huku tume ya uchaguzi ikiwasihi wananchi kuwa watulivu na kusubiri matangazo rasmi ya mwisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Patrick Nshindano.

Ikumbukwe serikali ya Zambia ilizima mtandao wa WhatsApp usiku wa kuamkia Jumamosi jambo lililotajwa na waangalizi wa uchaguzi kama kitendo cha kuzuia wananchi kuwa huru katika mawasiliano.

Aidha pia maswali yameibuka ni kwa nini serikali ya Zambia imewaweka mamia ya maafisa wa Kijeshi katika barabara kuu za Jiji la Lusaka. Haijabainika ni kitu gani kitafuata sasa baada ya serikali ya Rais Edgar Lungu kupinga matokeo ya uchaguzi.

Ni suala la kusubiria!

Kevin Ikaria.

Leave a Comment