Type to search

REAL MADRID KUJIONDOA LA LIGA, WANATAKA EPL.

Sports Swahili News

REAL MADRID KUJIONDOA LA LIGA, WANATAKA EPL.

Share

Vyanzo vya habari kutoka nchini Uhispania vimeripoti kwamba klabu ya Real Madrid inawaza kutuma ombi la kujiondoa katika ligi kuu ya Hispania LaLiga.

Rais wa klabu hiyo Florentino Perez anataka kuihamisha ligi kuu ya Uingereza EPL sababu kuu ikiwa ni tofauti za kibinafsi kati ya Perez na Rais wa La Liga Javier Tebas. Aidha pia kero la Perez la kutofanikisha wazo lake la awali la
kuunda SUPER LEAGUE, vilevile linachangia kutaka kuondoka LaLiga.

Gazeti la michezo la Mundo Deportivo limedokeza kuwa sio tu EPL ambayo Perez anatamani kujiunga nayo, lakini pia yupo radhi kuwasilisha ombi katika ligi ya Series A ya Italia na Bundesliga ya Ujerumani.

Ripoti hizi zimeibua maswali miongoni mwa mashabiki wengi wa soka ikizingatiwa kwamba Real Madrid ni klabu ya Uhispania – mchakato wa kuhamia ligi nyingine nje ya taifa la Uhispania itakuwaje ?

Leave a Comment