Type to search

SENATOR LINTURI ADAIWA KUTAKA KUMBAKA MWANAMKE NANYUKI.

Breaking News Swahili News trending News

SENATOR LINTURI ADAIWA KUTAKA KUMBAKA MWANAMKE NANYUKI.

Share

Seneta wa kaunti ya Meru Mithika Linturi amewasilisha ombi katika Mahakama akitaka zuio la kutokamatwa kufuatia madai ya ubakaji.

Inadaiwa Linturi alijaribu kumbaka mwanamke huyo katika hoteli ya Maiyan Villas mjini Nanyuki kaunti ya Laikipia tarehe 29, January 2021 baada ya mumewe kuondoka hotelini humo.

Hatahivyo Linturi anasema hana kumbukumbu ya tukio hilo na kuitaka Mahakama kuzuia kukamatwa kwake.
Mwanamke huyo(ambaye jina lake limebanwa) anadai aliacha mlango wa chumba chake wazi dakika chache tu baada ya mumewe kwenda matanuzi na rafiki, na ndipo seneta Linturi alipitiliza kimya-kimya akitaka kushiriki mapenzi naye.

“Saa tisa alfajiri mlango ulikuwa wazi tu na niliskia mtu akipitiliza. Nilidhani ni mume wangu kumbe ilikuwa seneta Linturi ambaye alisogea mpaka kitandani na kuanza kunipapasa.” Inasema ripoti ya mlalamishi.

Muda mchache mumewe alirudi na kumfumania Linturi kitandani na mkewe. Inasadikiwa Seneta Linturi alijitolea kuwapa wawili hao Ksh 200,000 pesa taslimu na hata baadae akatuma Ksh 800,000 za nyongeza.

Leave a Comment