Type to search

“Sisi Hatuwezi Kumchagulia Diamond Mpenzi” Esma Platnumz Ajibu Madai.

Entertainment Swahili News

“Sisi Hatuwezi Kumchagulia Diamond Mpenzi” Esma Platnumz Ajibu Madai.

Share

Diamond Platnumz ni msanii ambaye maisha yake ya mapenzi yamekuwa hayana mafanikio kama sanaa yake ya uimbaji. Hili limepelekea mashabiki wake kumpa jina ‘SIMBA WA EAST AFRICA’ kutokana na kwamba amezaa watoto na wanawake 3 tofauti kutoka Tanzania, Kenya na Uganda lakini hakuna aliyebahatika kuolewa na Diamond.

Hali halisi hii imepelekea baadhi ya watu kudai kwamba familia ya Diamond ndio kichocheo cha mahusiano yake kuvunjika. Hata hivyo dadake Diamond Platnumz amekanusha madai hayo akisema kakake ni mtu mzima mwenye maamuzi yake binafsi na kwa hivyo hawana sababu ya kuthubutu kumchagulia mpenzi.

“Kaka yangu sio mtoto, ni mtu mzima ambaye anajielewa, huwaleta wanawake wote nyumbani, tumewafahamu kupitia kwake. Lakini Hamisa ndiye nilimjua kwa maana alikuwa rafiki yangu,lakini walipopendana nilishangaa sana. Hatujawahi mchagulia mwanamke,tumeona ya kwamba endapo tuko karibu sana na wapenzi wake watu wengi hudhani kwamba huwa tunamchagulia wanawake”

Diamond Platnumz ni baba wa watoto 4 ila kwa sasa hana mpenzi baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake raia wa Kenya Tanasha Donna.

Leave a Comment