Type to search

Tiwa Savage Kuachia EP(extended playlist) Yake ‘Water and Garri’ Wiki Hii

Entertainment Swahili News trending News

Tiwa Savage Kuachia EP(extended playlist) Yake ‘Water and Garri’ Wiki Hii

Share

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Tiwa Savage ametangaza kuwa ataiachia EP(Extended Playlist) mpya ijulikanayo kama ‘Water and Garri’ Ijumaa ijayo tarehe 20,2021.

Tiwa amewatangazia mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, “Water and Garri kuachiwa Ijumaa ijayo”
aliandika Savage.

Aidha pia EP hiyo inaweza kufanyiwa ‘Pre-order’ kupitia iTunes, Spotify au hata Deezer.Tangazo la Tiwa kwenye Instagram kuhusiana na EP hiyo lilifanywa na Mchekeshaji Elsa Majimbo.

Tiwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike nyota zaidi kutoka Nigeria, Afrika ya Magharibi na bara la Afrika kwa jumla.
Baadhi ya tuzo alizowahi kushinda ni pamoja na

  •  Tuzo ya MTV ya msanii bora wa kike kutoka Africa 2018.
  • Tuzo tatu za AFRIMMA za msanii bora wa kike, wimbo bora na video bora mtawalia.

Hapa Afrika Mashariki Tiwa Savage amefanya kolabo kubwa na nyota wa Bongo flavor Diamond Platnumz – [ wimbo wa FIRE ].

Leave a Comment