Type to search

Trump Amtaka Biden Ajiuzulu

Politics Swahili News trending News

Trump Amtaka Biden Ajiuzulu

Share

Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump amemshauri Rais wa sasa Joe Biden kujiuzulu kwa kile alichokitaja kama utepetevu wa Serikali yake katika kushughulikia tatizo la taifa la Afghanistan.

Kauli ya Trump inakuja siku mbili tu baada ya wanamgambo wa Taliban kutwaa mji Mkuu wa Afghanistan Kabul na kupitiza mpaka katika Ikulu ya Rais.

Trump amesema ni jambo la kusikitisha sana  Taliban kutwaa miji mikubwa ya Afghanistan licha ya historia ndefu ya uwepo wa wanajeshi ya Marekani nchini humo.

Taliban wametekeleza mambo yote haya ikiwa imebaki wiki mbili tu kabla ya tarehe ya mwisho ya Jeshi la Marekani
kuondoka nchini Afghanistan.

Hata hivyo, ni vyema ifahamike kuwa mchakato wa kuwaondoa Wanajeshi wa Marekani nchi Afghanistan ulianza katika utawala wa Trump kufuatia makubaliano yaliyoafikiwa Doha Qatar, lakini alipoingia Joe Biden, mchakato huo uliharakishwa na kusogezwa mbele.

Trump amesema kusogezwa mbele huko ndiyo kichocheo kikubwa cha vitendo vya Taliban kutwaa miji mikubwa ya
Afghanistan, “Wamuzi wa Rais Biden kuondoa Jeshi letu Afghanistan bila taratibu za msingi kuzingatiwa ipasavyo itabaki kuwa moja ya maanguko mabaya katika historia ya Marekani” alisema Trump tarehe 15 Agosti 2021.

Leave a Comment