Type to search

WANAMGAMBO WA TALIBAN WAANZA KUINGIA KABUL.

Politics Swahili News

WANAMGAMBO WA TALIBAN WAANZA KUINGIA KABUL.

Share

Hali ni tete nchini Afghanistan na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla baada ya waasi wa Afghanistan wenye msimamo mkali kutwaa miji mikubwa nchini humo na sasa hivi tayari wameanza kuingia maeneo yaliyopo karibu na
mji Mkuu wa Afghanistan Kabul.

Mataifa mengi yakiwemo Uingereza na Marekani tayari wametuma helikopta za kijeshi kuokoa wanadiplomasia wao waishio katika Jiji la Kabul.

Taliban wamesisitiza kuwa hawana haja na umwagikaji damu wa raia wasiokuwa na hatia lakini wamewaomba maafisa wa serikali – polisi na Jeshi wajisalimishe. Tayari wapo askari waliojisalimisha huku mashambulizi ya Taliban yakiendelea kusikika katika viunga vilivyopo karibu na Jiji kuu la Kabul.

Serikali ya Afghanistan kwa sasa imebaki tu na Jiji la Kabul na Jalalabad na inasadikiwa muda sio mrefu miji yote hiyo kubwa zaidi nchini humo itakuwa mikononi wa wapiganaji wa Taliban.

Haijabainika hasa ni vipi mchakato wa Uongozi wa Afghanistan utakavyoendelea iwapo Taliban watafanikiwa katika lengo lao la kuifurusha serikali. Hatahivyo, kiongozi wa ngazi ya juu ya Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar amesema watawasamehe maafisa wa serikali iwapo watajisalimisha kwao.  Vile vile Taliban wamewashauri wanawake kukimbilia maeneo ya mbali yaliyo salama zaidi.

Kevin Ikaria.

Leave a Comment