Type to search

Waziri Mkuu Wa Malaysia Ajiuzulu

Politics trending News

Waziri Mkuu Wa Malaysia Ajiuzulu

Share

Waziri Mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yassin amewasilisha waraka wa kujiuzulu kwa Mfalme Al Sultan Abdullah. Aidha pia Baraza Zima la Mawaziri limeacha kazi.

Wamuzi huu wa kujiuzulu unakuja wiki chache tu baada ya Muhyiddin kupoteza uungwaji mkono wa walio-wengi
katika Bunge. Aidha Muhyiddin amekuwa chini ya shinikizo zito la kujiuzulu. Ikumbukwe Waziri Mkuu huyo
alichukua hatamu ya Uongozi mwezi Machi 2020.

Haijabainika wazi ni nani sasa atakuwa Waziri Mkuu mpya ikizingatiwa kwamba hakuna Kiongozi mwenye
idadi nzuri ya walio wengi kwenye Bunge.

Hatahivyo, Mfalme Al Sultan Abdullah anayo nguvu ya kumteua yeyote katika Bunge anayedhaniwa kupata uungwaji mkono wa Wabunge.

Kuna hofu ya ni jinsi gani mchakato wa Uongozi utakavyoendeshwa sasa ikizingatiwa uchumi wa taifa hilo umedorora pakubwa kutokana na athari za janga la virusi vya Covid19.

Leave a Comment