Type to search

Yemi Alade Aachia EP Yake Mpya.

Entertainment Swahili News trending News

Yemi Alade Aachia EP Yake Mpya.

Share

Nyota wa muziki kutokea nchini Nigeria, Yemi Alade ameachia rasmi EP (Extended Playlist) yake mpya ijulikanayo kama “Queen Don Com” ambayo tayari ipo katika Soko la muziki.

‘Queen Don Com’ ina jumla ya nyimbo 7 na wala hakuna kolabo hata moja. Nyimbo hizo ni “Ogogoro”, “Sweety”, “Ike”, “Enjoyment”, “Dada”, “Ella” na “Fire”.

Yemi Alade amejishindia tuzo kadhaa kutokana na kazi zake za muziki kama vile AFRIMMA mwaka wa 2015 na 2018 katika kipengele cha msanii bora wa kike kutokea Afrika ya Magharibi.

Aidha pia Yemi Alade aliwahi kutwaa tuzo ya MTV mwaka 2015 na 2016 katika kipengele cha msanii bora wa kike kutokea bara la Afrika.

Leave a Comment